Aal-i-Imraan 3:109
آل عمرانوَلِلَّهِ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ ۚ وَإِلَى ٱللَّهِ تُرْجَعُ ٱلْأُمُورُ
Na ni cha Mwenyezi Mungu kilicho katika mbingu na kilicho katika ardhi, na kwa Mwenyezi Mungu ndiko mambo yote yatarejeshwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kila kilichomo Mbinguni na kilichomo Ardhini ni cha Mwenyezi Mungu; na mambo yote yatarejea kwa Mwenyezi Mungu. [109]
[109] Na vyote viliomo Mbinguni na Ardhini ni vya Mwenyezi Mungu peke yake, ni vyake kwa kuviumba, na kuvimiliki, na kuvisarifu. Na marejeo ya mambo yao ni kwake Yeye. Kwa hivyo humlipa kila mmoja kama anavyo stahiki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na ni Vyake, Yeye Allah Mtukufu Peke Yake, vyote vilivyo mbinguni na vilivyo ardhini, ni milki Yake Pekee kwa kuviumba na kuvisimamia. Na marejeo ya viumbe wote ni Kwake Yeye Peke Yake, na Atamlipa kila mmoja kwa kadiri anayostahiki.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net