Aal-i-Imraan 3:108
آل عمرانتِلْكَ ءَايَـٰتُ ٱللَّهِ نَتْلُوهَا عَلَيْكَ بِٱلْحَقِّ ۗ وَمَا ٱللَّهُ يُرِيدُ ظُلْمًا لِّلْعَـٰلَمِينَ
Hizi ni Aya za Mwenyezi Mungu tunazokusomea kwa haki. Na Mwenyezi Mungu hataki kuwadhulumu walimwengu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hizi ni Aya za Mwenyezi Mungu tunakusomea kwa haki. Na Mwenyezi Mungu hataki kuwadhulumu walimwengu. [108]
[108] Na hizo Aya zilizo kuja za kueleza kuwa mwema na mwovu watalipwa tunakusomea, nazo zimekusanya haki na uadilifu. Na Mwenyezi Mungu hataki kumdhulumu yeyote kati ya watu na majini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hizi ni aya za Allah Mtukufu na hoja Zake zenye kung’ara, tunakusomea na kukusimulia, ewe Mtume, kwa ukweli na yakini. Na Allah Mtukufu Hakuwa ni mwenye kumdhulumu yoyote katika viumbe Wake wala si mwenye kupunguza chochote katika vitendo vyao, kwani Yeye ni Hakimu Mwenye uadilifu Asiyedhulumu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net