Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 107

Aal-i-Imraan 3:107

آل عمران

وَأَمَّا ٱلَّذِينَ ٱبْيَضَّتْ وُجُوهُهُمْ فَفِى رَحْمَةِ ٱللَّهِ هُمْ فِيهَا خَـٰلِدُونَ

Maana

Na ama wale ambao nyuso zao zitakuwa nyeupe, basi watakuwa katika rehema ya Mwenyezi Mungu. Wao humo watadumu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ama wale ambao nyuso zao zitanawiri watakuwa katika rehema ya Mwenyezi Mungu. Wao humo watadumu. [107]

[107] Ama wale nyuso zao zimekuwa nyeupe, yaani zimenawiri, kwa kufurahi, hao watakuwa katika Pepo ambayo Mwenyezi Mungu amewapa kwa rehema yake, wadumu humo milele.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ama wale ambao nyuso zao zitakuwa nyeupe kwa mn’garo wa neema na kwa yale mema ambayo walipewa bishara nayo, wao watakuwa katika Pepo ya Allah Mtukufu na starehe zake. Wao watasalia humo, hawatatoka humo milele.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net