Al-Ankaboot 29:53
العنكبوتوَيَسْتَعْجِلُونَكَ بِٱلْعَذَابِ ۚ وَلَوْلَآ أَجَلٌ مُّسَمًّى لَّجَآءَهُمُ ٱلْعَذَابُ وَلَيَأْتِيَنَّهُم بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ
Na wanakuhimiza waletewe adhabu kwa haraka. Na lau kuwa hapana wakati maalumu uliowekwa, basi adhabu ingeliwajia, na ingeliwatokea kwa ghafla ilhali wao hawana habari.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wanakuhimiza waletewe adhabu kwa haraka. Na lau kuwa hapana wakati maalumu ulio wekwa, basi adhabu ingeli wajia, na ingeli watokea kwa ghafla, na hali wao hawana khabari.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wanakuharakisha, ewe Mtume, hawa washirikina wa watu wako uwaletee adhabu kwa kukufanyia shere. Na lau si Allah Mtukufu kuwa Amewawekea wakati wa kuadhibiwa wao duniani usiotangulia wala kuchelewa, ingewajia adhabu pale walipoitaka. Na kwa hakika itawajia ghafla na hali wao hawaitambui wala kuihisi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net