Al-Ankaboot 29:52
العنكبوتقُلْ كَفَىٰ بِٱللَّهِ بَيْنِى وَبَيْنَكُمْ شَهِيدًا ۖ يَعْلَمُ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۗ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ بِٱلْبَـٰطِلِ وَكَفَرُوا۟ بِٱللَّهِ أُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْخَـٰسِرُونَ
Sema, "Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni Shahidi kati yangu na nyinyi. Anayajua yaliyo katika mbingu na ardhi. Na wale wanaoiamini batili na wakamkufuru Mwenyezi Mungu, hao ndio waliohasiri."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni Shahidi baina yangu na nyinyi. Anayajua yaliomo katika mbingu na ardhi. Na wale wanao amini upotovu na wakamkataa Mwenyezi Mungu, hao ndio walio khasiri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, Inatosha kuwa Allah Mtukufu ni Shahidi baina yangu mimi na nyinyi juu ya ukweli wangu wa kuwa mimi ni Mtume Wake, na juu ya kunikanusha kwenu mimi na kuirudisha kwenu haki niliyokuja nayo kutoka kwa Allah Mtukufu. Anavijuwa vilivyomo mbinguni na ardhini», hakuna kinachofichamana na Yeye chochote kile kilichoko ndani ya hivyo viwili. Na wale waliouamini urongo na wakamkanusha Allah Mtukufu, pamoja na kuwepo dalili hizi zilizo wazi, hao ndiyo wenye hasara ulimwenguni na Akhera.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net