Al-Ankaboot 29:46
العنكبوتوَلَا تُجَـٰدِلُوٓا۟ أَهْلَ ٱلْكِتَـٰبِ إِلَّا بِٱلَّتِى هِىَ أَحْسَنُ إِلَّا ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ مِنْهُمْ ۖ وَقُولُوٓا۟ ءَامَنَّا بِٱلَّذِىٓ أُنزِلَ إِلَيْنَا وَأُنزِلَ إِلَيْكُمْ وَإِلَـٰهُنَا وَإِلَـٰهُكُمْ وَٰحِدٌ وَنَحْنُ لَهُۥ مُسْلِمُونَ
Wala msijadiliane na Watu wa Kitabu isipokuwa kwa njia iliyo nzuri kabisa, isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao. Na semeni, "Tumeyaamini yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwenu. Na mungu wetu na mungu wenu ni Mmoja. Na sisi ni wenye kusilimu kwake."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala msijadiliane na Watu wa Kitabu ila kwa njia iliyo nzuri kabisa, isipo kuwa wale walio dhulumu miongoni mwao. Na semeni: Tumeyaamini yaliyo teremshwa kwetu na yaliyo teremshwa kwenu. Na Mungu wetu na Mungu wenu ni Mmoja. Na sisi ni wenye kusilimu kwake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wala msijadiliane, enyi Waumini, na Mayahudi na manaswara isipokuwa kwa njia nzuri na maneno mazuri na kulingania kwenye haki kwa njia nyepesi yenye kupelekea kwenye lengo hilo, isipokuwa wale ambao wamekaa kando na haki wakafanya ushindani na kiburi na wakatangaza vita juu yenu, basi hao piganeni nao kwa upanga mpaka waamini au watoe jizia (kodi maalumu) kwa mkono na wao wakiwa katika hali ya unyonge. Na semeni, «Tumeiamini Qur’ani iliyoteremshwa kwetu, na tumeiamini Taurati na Injili ambazo mliteremshiwa, na Mola wetu na Mola wenu ni Mmoja Hana mshirika Wake katika uungu Wake, wala katika sifa Yake ya kuwa ni Mola, wala majina Yake na sifa Zake. Na sisi ni wenye kunyenyekea na kuwa wanyonge Kwake kwa kumtii katika yale Aliyotuamrisha na Aliyotukataza».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net