Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 29 · Aya ya 47

Al-Ankaboot 29:47

العنكبوت

وَكَذَٰلِكَ أَنزَلْنَآ إِلَيْكَ ٱلْكِتَـٰبَ ۚ فَٱلَّذِينَ ءَاتَيْنَـٰهُمُ ٱلْكِتَـٰبَ يُؤْمِنُونَ بِهِۦ ۖ وَمِنْ هَـٰٓؤُلَآءِ مَن يُؤْمِنُ بِهِۦ ۚ وَمَا يَجْحَدُ بِـَٔايَـٰتِنَآ إِلَّا ٱلْكَـٰفِرُونَ

Maana

Na namna hivyo tumekuteremshia Kitabu hiki (Qur-ani). Basi wale tuliowapa Kitabu (cha Biblia) wataiamini (Qur-ani), na miongoni mwa hawa (washirikina) wapo watakaoiamini. Na hawazikatai Ishara zetu isipokuwa makafiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na namna hivi tumekuteremshia Kitabu (cha Qur'ani). Basi wale tulio wapa Kitabu (cha Biblia) wataiamini (Qur'ani), na miongoni mwa hawa (washirikina) wapo watakao iamini. Na hawazikatai Ishara zetu isipo kuwa makafiri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kama tulivyowateremshia Kitabu, ewe Mtume, wale Mitume waliokuwa kabla yako, vilevile tumekuteremshia Kitabu hiki chenye kusadikisha Vitabu vilivyotangulia. Basi wale tuliyowapa Kitabu miongoni mwa Wana wa Isrãîl wakamjua vile inavyotakikana wamjue, wanaiamini Qur’ani. Na kati ya hawa Warabu wa Kikureshi kuna wanaomuamini. Na hawaikanushi Qur’ani au kuzifanyia shaka dalili zake na hoja zake zenye ushahidi uliyo wazi isipokuwa makafiri ambao mienendo yao ni kukataa na kufanya ushindani.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ankaboot

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net