Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 29 · Aya ya 45

Al-Ankaboot 29:45

العنكبوت

ٱتْلُ مَآ أُوحِىَ إِلَيْكَ مِنَ ٱلْكِتَـٰبِ وَأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ ۖ إِنَّ ٱلصَّلَوٰةَ تَنْهَىٰ عَنِ ٱلْفَحْشَآءِ وَٱلْمُنكَرِ ۗ وَلَذِكْرُ ٱللَّهِ أَكْبَرُ ۗ وَٱللَّهُ يَعْلَمُ مَا تَصْنَعُونَ

Maana

Soma yale uliyofunuliwa katika Kitabu, na ushike Swala. Hakika Swala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini kumdhukuru Mwenyezi Mungu ndilo jambo kubwa kabisa. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayoyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

SOMA uliyo funuliwa katika Kitabu, na ushike Swala. Hakika Swala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini kumdhukuru Mwenyezi Mungu ndilo jambo kubwa kabisa. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayo yatenda.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Isome hii Qur’ani iliyoteremshwa kwako, na uifuate kivitendo, na utekeleze Swala kwa mipaka yake, kwani utunzaji wa Swala unamkataza mtu kuingia kwenye vitendo vya uasi na makatazo. Hivyo ni kwamba mwenye kuzitimiza nguzo zake na masharti yake, moyo wake unang’ara, Imani yake inazidi, hima yake ya kufanya mema inapata nguvu na matamanio yake ya kufanya mabaya yanapungua au yanaondoka. Na kwa hakika, kumtaja Allah Mtukufu katika Swala na isiyokuwa Swala ni jambo kubwa na bora kuliko kitu chochote. Na Allah Mtukufu Anayajua mnayoyatenda ya uzuri na ubaya, hivyo basi Atawalipa kwa hayo malipo makamilifu zaidi na yanayotosha zaidi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ankaboot

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net