Al-Ankaboot 29:32
العنكبوتقَالَ إِنَّ فِيهَا لُوطًا ۚ قَالُوا۟ نَحْنُ أَعْلَمُ بِمَن فِيهَا ۖ لَنُنَجِّيَنَّهُۥ وَأَهْلَهُۥٓ إِلَّا ٱمْرَأَتَهُۥ كَانَتْ مِنَ ٱلْغَـٰبِرِينَ
Akasema, "Hakika humo yumo Luti." Wao wakasema, "Sisi tunajua zaidi ni nani yumo humo. Hapana shaka tutamwokoa yeye na ahali zake, isipokuwa mkewe aliye miongoni mwa watakaokaa nyuma."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akasema: Hakika humo yumo Luut'i. Wao wakasema: Sisi tunajua zaidi nani yumo humo. Hapana shaka tutamwokoa yeye na ahali zake, isipo kuwa mkewe aliye miongoni mwa watao kaa nyuma.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Akasema Ibrãhîm kuwaambia Malaika, «Huko kuna Lûṭ, na yeye si miongoni mwa madhalimu.» Malaika wakasema, Sisi tunamjua zaidi aliye huko. Tutamuokoa, yeye na watu wa nyumbani kwake, na maangamivu yatakayowashukia watu wa kijiji chake, isipokuwa mke wake atakayesalia kwenye maangamivu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net