Al-Ankaboot 29:31
العنكبوتوَلَمَّا جَآءَتْ رُسُلُنَآ إِبْرَٰهِيمَ بِٱلْبُشْرَىٰ قَالُوٓا۟ إِنَّا مُهْلِكُوٓا۟ أَهْلِ هَـٰذِهِ ٱلْقَرْيَةِ ۖ إِنَّ أَهْلَهَا كَانُوا۟ ظَـٰلِمِينَ
Na wajumbe wetu walipomjia Ibrahim na bishara, walisema, "Hakika sisi hapana shaka tutawaangamiza watu wa mji huu, kwani watu wake hakika wamekuwa madhalimu."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wajumbe wetu walipo mjia Ibrahim na bishara, walisema: Hakika sisi hapana shaka tutawahiliki watu wa mji huu, kwani watu wake hakika wamekuwa madhaalimu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Malaika walipomjia Ibrãhîm na habari ya furaha itokayo kwa Allah Mtukufu ya (kuzaliwa) Isḥāq, na nyuma ya Isḥãq ni mwanawe, Ya‛qûb, walisema wale Malaika, «Sisi ni wenye kuwaangamiza watu wa kijiji cha watu wa Lûṭ, nacho ni Sadūm, kwa kuwa watu wake wamekuwa ni wenye kujidhulumu wenyewe kwa kumuasi Allah Mtukufu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net