Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 29 · Aya ya 33

Al-Ankaboot 29:33

العنكبوت

وَلَمَّآ أَن جَآءَتْ رُسُلُنَا لُوطًا سِىٓءَ بِهِمْ وَضَاقَ بِهِمْ ذَرْعًا وَقَالُوا۟ لَا تَخَفْ وَلَا تَحْزَنْ ۖ إِنَّا مُنَجُّوكَ وَأَهْلَكَ إِلَّا ٱمْرَأَتَكَ كَانَتْ مِنَ ٱلْغَـٰبِرِينَ

Maana

Na wajumbe wetu walipomfikia Luti, alihuzunika kwa sababu yao, na moyo ukaona dhiki kubwa kwa sababu yao. Wakasema, "Usihofu, wala usihuzunike. Hakika sisi tutakuokoa wewe na ahali zako, isipokuwa mkeo aliye miongoni mwa watakaokaa nyuma.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wajumbe wetu walipo mfikia Luut'i, alihuzunika kwa ajili yao, na moyo uliona dhiki kwa ajili yao. Wakasema: Usiogope, wala usihuzunike. Hakika sisi tutakuokoa wewe na ahali zako, ila mkeo aliye miongoni mwa watao kaa nyuma.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Malaika walipomjia Lûṭ, hilo lilimkera, kwa kuwa yeye aliwadhania ni wageni wanadamu na akaingiwa na masikitiko kwa kuwako kwao kwa kuwa ajua ubaya wa kitendo cha watu wake, na wao wakamwambia, «Usituogopee, kwani watu wako hawatatufikia. Na wala usiwe na masikitiko kwa kuwa tunakupasha habari kuwa sisi ni wenye kuwaangamiza wao. Sisi ni wenye kukuokoa wewe na hiyo adhabu itakayowashukia watu wako na ni wenye kuwaokoa watu wa nyumbani kwako pamoja nawe isipokuwa mke wako, kwani yeye ni mwenye kuangamia akiwa na wale wenye kuangamia katika watu wake».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ankaboot

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net