Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 29 · Aya ya 18

Al-Ankaboot 29:18

العنكبوت

وَإِن تُكَذِّبُوا۟ فَقَدْ كَذَّبَ أُمَمٌ مِّن قَبْلِكُمْ ۖ وَمَا عَلَى ٱلرَّسُولِ إِلَّا ٱلْبَلَـٰغُ ٱلْمُبِينُ

Maana

Na mkikadhibisha, basi kaumu kadhaa wa kadhaa za kabla yenu zilikwisha kadhibisha. Na si juu ya Mtume isipokuwa kufikisha Ujumbe waziwazi."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mkikadhibisha, basi kaumu kadhaa wa kadhaa za kabla yenu zilikwisha kadhibisha. Na si juu ya Mtume ila kufikisha Ujumbe waziwazi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mkimkanusha, enyi watu, Mtume wetu Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), katika kile alichowalingania mkifuate cha kumuabudu Allah Mtukufu Peke Yake, basi kuna makundi ya watu kabla yenu waliowakanusha Mitume wao katika kile walichowaitia, na kwa hivyo zikawashukia hasira za Allah Mtukufu. Na Mtume Muhammad hana jukumu lingine isipokuwa ni kuwafikishia nyinyi kutoka kwa Allah Mtukufu ujumbe Wake ufikishaji wenye uwazi, na ashafanya hilo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ankaboot

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net