Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 29 · Aya ya 17

Al-Ankaboot 29:17

العنكبوت

إِنَّمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ أَوْثَـٰنًا وَتَخْلُقُونَ إِفْكًا ۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ تَعْبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ لَا يَمْلِكُونَ لَكُمْ رِزْقًا فَٱبْتَغُوا۟ عِندَ ٱللَّهِ ٱلرِّزْقَ وَٱعْبُدُوهُ وَٱشْكُرُوا۟ لَهُۥٓ ۖ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ

Maana

Hakika nyinyi mnaabudu tu masanamu badala ya Mwenyezi Mungu, na mnazua uzushi. Hakika hao mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu hawawamilikii riziki yoyote. Basi tafuteni riziki kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na mumuabudu Yeye, na mumshukuru Yeye. Kwake Yeye ndiko mtarudishwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika nyinyi mnaabudu masanamu badala ya Mwenyezi Mungu, na mnazua uzushi. Hakika hao mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu hawakumilikiini riziki yoyote. Takeni riziki kwa Mwenyezi Mungu, na mumuabudu Yeye, na mumshukuru Yeye. Kwake Yeye ndio mtarudishwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hamuabudu, enyi watu, badala ya Allah Mtukufu isipokuwa masanamu na mnazua urongo kwa kuwaita wao waungu. Kwa hakika, hawa masanamu wenu mnaoaowaabudu badala ya Allah Mtukufu, hawawezi kuwaruzuku nyinyi kitu chochote, basi tafuteni riziki kwa Allah Mtukufu na sio kwa masanamu wenu na mumtakasie ibada na shukrani kwa kuwaruzuku. Ni kwa Allah Mtukufu mtarudishwa baada ya kufa kwenu, na hapo awalipe kwa yale ambayo mlifanya.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ankaboot

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net