Al-Ankaboot 29:16
العنكبوتوَإِبْرَٰهِيمَ إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ ٱعْبُدُوا۟ ٱللَّهَ وَٱتَّقُوهُ ۖ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ
Na Ibrahim pale alipowaambia watu wake, "Muabuduni Mwenyezi Mungu, na mcheni Yeye. Hiyo ndiyo heri yenu, ikiwa nyinyi mnajua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Ibrahim pale alipo waambia watu wake: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na mcheni Yeye. Hiyo ndiyo kheri yenu, ikiwa nyinyi mnajua.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kumbuka ewe Mtume, Ibrãhîm, amani imshukie, alipowalingania watu wake kwamba: mtakasieni Ibada Allah Mtukufu Peke Yake, na muogope hasira Zake kwa kutekeleza faradhi Zake na kujiepusha na vitendo vya kumuasi. Hilo ni bora kwenu ikiwa mnakijua kilicho chema kwenu kutokana na kilicho kibaya kwenu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net