Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 29 · Aya ya 19

Al-Ankaboot 29:19

العنكبوت

أَوَلَمْ يَرَوْا۟ كَيْفَ يُبْدِئُ ٱللَّهُ ٱلْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥٓ ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٌ

Maana

Je, wao hawaoni jinsi Mwenyezi Mungu anavyoanzisha uumbaji, na kisha akaurudisha tena. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Wao hawaoni jinsi Mwenyezi Mungu anavyo anzisha uumbaji, na kisha akarudisha tena. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwani hawa hawajui ni vipi Allah Mtukufu Anaanzisha uumbaji viumbe kutoka katika hali ya kutokuwako, kisha Atawarudisha baada ya kutoweka kwao, kama alivyoanzisha mara ya kwanza uumbaji mpya na kwamba kulifanya hili si jambo linalomshinda? Hakika hilo kwa Allah Mtukufu ni lepesi kama lilivyokuwa lepesi lile la kuanzisha uumbaji wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ankaboot

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net