Al-Qasas 28:9
القصصوَقَالَتِ ٱمْرَأَتُ فِرْعَوْنَ قُرَّتُ عَيْنٍ لِّى وَلَكَ ۖ لَا تَقْتُلُوهُ عَسَىٰٓ أَن يَنفَعَنَآ أَوْ نَتَّخِذَهُۥ وَلَدًا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ
Na mkewe Firauni alisema, "Atakuwa kiburudisho cha macho yangu na yako. Msimuuwe! Huenda akatufaa, au tumpange kuwa mwenetu." Wala wao hawakutambua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mkewe Firauni alisema: Atakuwa kiburudisho cha macho kwangu na kwako. Msimuuwe! Huenda akatufaa, au tumpange kuwa mwenetu. Wala wao hawakutambua. [9]
[9] Mke wa Firauni alipo mwona mtoto alimwambia mumewe: Mtoto huyu atatuletea furaha mimi na wewe. Tumweke, tusimuuwe, kwa kutaraji kuwa atakuja tufaa kuendesha mambo yetu. Au tumfanye mwenetu wa kumlea. Na wao kumbe hawatambui aliyo mkadiria Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na mke wa Firáwn alipomuona, Allah Mtukufu Alimtia mapenzi moyoni mwake na akasema kuhusu Firáwn, «Mtoto huyu atakuwa chimbuko la furaha kwangu mimi na wewe, Msimuue kwani huenda tukapata kheri kutoka kwake au tumfanye ni mtoto wetu» na hali Firáwn na jamaa wa nyumbani kwake hawafahamu kwamba maangamivu yao yatatokana mikononi mwake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net