Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 10

Al-Qasas 28:10

القصص

وَأَصْبَحَ فُؤَادُ أُمِّ مُوسَىٰ فَـٰرِغًا ۖ إِن كَادَتْ لَتُبْدِى بِهِۦ لَوْلَآ أَن رَّبَطْنَا عَلَىٰ قَلْبِهَا لِتَكُونَ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ

Maana

Na (ufahamu wa) moyo wa mama yake Musa ukawa mtupu. Alikuwa karibu kumdhihirisha, ingelikuwa hatukumtia nguvu moyo wake ili awe miongoni mwa Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na moyo wa mama yake Musa ukawa mtupu. Alikuwa karibu kumdhihirisha, ingeli kuwa hatukumtia nguvu moyo wake ili awe miongoni mwa Waumini. [10]

[10] Na mama yake Musa akawa hajitambui kwa dhiki iliyo muingia kwa kuwa mwanawe kaangukia mikononi mwa Firauni. Akawa anakurubia kujitambulisha kwamba yeye ndiye mama yake. Lau ingeli kuwa Mwenyezi Mungu hakuutia imara moyo wake kwa kusubiri, basi angeli tangaza kuwa huyo ni mwanawe, jinsi alivyo kuwa akimhurumia, na pia ili awe miongoni mwa Waumini wenye kutulia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kifua cha mama yake Mûsã kikawa hakijishughulishi na kitu chochote duniani isipokuwa hamu ya Mûsã na kumtaja, na alikaribia kudhihirisha kuwa yule ni mwanawe lau si sisi kumthibitisha, naye akavumilia asilidhihirishe hilo, ili awe ni miongoni mwa wenye kuamini ahadi ya Allah Mtukufu na mwenye kuwa na yakini nayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net