Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 11

Al-Qasas 28:11

القصص

وَقَالَتْ لِأُخْتِهِۦ قُصِّيهِ ۖ فَبَصُرَتْ بِهِۦ عَن جُنُبٍ وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ

Maana

Naye akamwambia dada yake Musa, "Mfuatie." Basi naye akawa anamuangalia kwa mbali bila ya wao kujua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Naye akamwambia dada yake Musa: Mfuatie. Basi naye akawa anamuangalia kwa mbali bila ya wao kujua. [11]

[11] Yule mama akamwambia dada yake Musa: Mfuatie upate kujua khabari zake. Basi akawa anamwona kwa mbali na anatahadhari asitambulikane, na Firauni na watu wake wakawa hawajui kama yule ni dada yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na akasema mama yake Mûsã kumwambia nduguye wa kike alipomtupa mtoni, «Fuata athari za Mûsã uone atafanywa nini? Akafuata athari zake na akamuona kwa mbali na hali watu Firáwn hawajui kwamba yeye ni dada yake na kwamba yeye afuatilia habari zake».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net