Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 12

Al-Qasas 28:12

القصص

وَحَرَّمْنَا عَلَيْهِ ٱلْمَرَاضِعَ مِن قَبْلُ فَقَالَتْ هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَىٰٓ أَهْلِ بَيْتٍ يَكْفُلُونَهُۥ لَكُمْ وَهُمْ لَهُۥ نَـٰصِحُونَ

Maana

Na tukamjaalia awakatae wanyonyeshaji wote tangu mwanzo. Kwa hivyo, dada yake akasema, "Je, niwaonyesheni watu wa nyumba watakaomlelea huyu, nao pia watakuwa wema kwake?"

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tukamjaalia awakatae wanyonyeshaji wote tangu mwanzo, mpaka dada yake akasema: Je! Nikuonyesheni watu wa nyumba watakao mlea kwa ajili yenu, nao pia watakuwa wema kwake? [12]

[12] Mwenyezi Mungu alimjaalia yule mtoto akatae ziwa la kila mnyonyeshaji kabla hawajamjia mama yake. Watu wa Firauni wakaingiwa na ghamu, na wakashughulishwa na hayo. Yule dada yake ndio akawaambia: Nikuongozeni kwenye ukoo utakao muangalia huyu mtoto, na kumnyonyesha, na kumlea, nao watamtazama vizuri?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na tulimzuia Mûsã asinyonye kutoka kwa wanyonyeshaji kabla hatujamrudisha kwa mama yake, hapo dada yake akasema, «Je, ni waonyeshe watu wa nyumba ambao watamlea na kumnyonyesha vizuri na ambao watakuwa na huruma naye? Wakamkubalia hilo».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net