Al-Qasas 28:13
القصصفَرَدَدْنَـٰهُ إِلَىٰٓ أُمِّهِۦ كَىْ تَقَرَّ عَيْنُهَا وَلَا تَحْزَنَ وَلِتَعْلَمَ أَنَّ وَعْدَ ٱللَّهِ حَقٌّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ
Basi tukamrudisha kwa mama yake ili macho yake yaburudike, wala asihuzunike. Na ajue ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli, lakini wengi wao hawajui.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi tukamrudisha kwa mama yake ili macho yake yaburudike, wala asihuzunike. Na ajue ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli, lakini wengi wao hawajui. [13]
[13] Wakaukubali uwongozi wake, na Mwenyezi Mungu akamrudisha kwa mama yake, ili nafsi yake itue, na afurahi kwa kurudi kwake, wala asihuzunike kwa kuwa mbali naye, na ili azidi kujua ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu aliyo mpa kuwa atamrudishia imetimia wala hayendi kinyume. Lakini watu wengi walikuwa hawajui kurudi Musa kwa mama yake, kwani hayo yote yalifichikana kwao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi tukamrudisha Mûsã kwa mama yake, ili jicho lake litulie kwake na tukamtekelezea ahadi yetu kwake, kwa kuwa alirudi kwake akiwa amesalimika na kuuawa na Firáwn, na ili asihuzunike kwa kuwa mbali naye, na ajue kwamba ahadi ya Allah Mtukufu ni kweli, ile Aliyowaahidi kuwa atamrudishia na Amfanye ni miongoni mwa Mitume. Hakika Allah Mtukufu Haendi kinyume na ahadi Yake, lakini wengi wa washirikina hawajui kwamba ahadi ya Allah Mtukufu ni kweli.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net