Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 8

Al-Qasas 28:8

القصص

فَٱلْتَقَطَهُۥٓ ءَالُ فِرْعَوْنَ لِيَكُونَ لَهُمْ عَدُوًّا وَحَزَنًا ۗ إِنَّ فِرْعَوْنَ وَهَـٰمَـٰنَ وَجُنُودَهُمَا كَانُوا۟ خَـٰطِـِٔينَ

Maana

Basi wakamwokota watu wa Firauni, aje kuwa adui kwao na huzuni. Hakika Firauni na Hamana na majeshi yao walikuwa wenye makosa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi wakamwokota watu wa Firauni, aje kuwa adui kwao na huzuni. Hakika Firauni na Hamana na majeshi yao walikuwa wenye makosa. [8]

[8] Watu wa Firauni wakamchukua, ili aliyo kadiria Mwenyezi Mungu yatimie, yaani Musa apate kuwa Mtume mwenye kuwapinga wao, na mwenye kuwaletea huzuni, kwa kuitoa kombo dini yao na kuishambulia dhulma yao. Hakika Firauni na Hamana na wasaidizi wao walikuwa ni watu wenye madhambi, walio pindukia mipaka katika ujeuri na uharibifu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hapo akamuweka sandukuni na akalitupa kwenye mto wa Nail, na wafuasi wa Firáwn wakalipata na wakalichukua, na mwisho wake ukawa vile Alivyokadiria Allah Mtukufu kuwa Mûsã awe ni adui yao kwa kuwa kinyume na dini yao, na awatie kwenye huzuni ya kuzamishwa na kuondokewa na ufalme wao mikononi mwake. Kwa hakika, Firáwn na Hāmān na wasaidizi wao walikuwa wafanyaji makosa washirikina.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net