Al-Qasas 28:7
القصصوَأَوْحَيْنَآ إِلَىٰٓ أُمِّ مُوسَىٰٓ أَنْ أَرْضِعِيهِ ۖ فَإِذَا خِفْتِ عَلَيْهِ فَأَلْقِيهِ فِى ٱلْيَمِّ وَلَا تَخَافِى وَلَا تَحْزَنِىٓ ۖ إِنَّا رَآدُّوهُ إِلَيْكِ وَجَاعِلُوهُ مِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ
Tulimfunulia mama yake Musa kwa kumwambia: Mnyonyeshe. Na utakapomhofia, basi mtie mtoni, na usihofu wala usihuzunike. Hakika Sisi tutamrudisha kwako na tutamfanya miongoni mwa Mitume.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Tulimfunulia mama yake Musa kwa kumwambia: Mnyonyeshe. Na utakapo mkhofia basi mtie mtoni, na usikhofu wala usihuzunike. Hakika Sisi tutamrudisha kwako na tutamfanya miongoni mwa Mitume. [7]
[7] Na Mwenyezi Mungu alimfahamisha mama yake Musa, alipo kuwa anamkhofia asichinjwe na Firauni kama alivyo kuwa akiwachinja watoto wanaume wa Bani Israili, kwamba amnyonyeshe kwa kituo na hatauliwa na Firauni. Ikiwa anaogopa asije kutambulikana amtie katika sanduku, na amtie katika mto wa Nile bila ya khofu wala huzuni. Kwani bila ya shaka Mwenyezi Mungu amedhamini kumhifadhi na kumrejeshea mwenyewe, na kumtuma kwa Wana wa Israili.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tukampa mawazo mamake Mûsã alipomzaa na akamuogopea asije Firáwn akamchinja kama anavyowachinja watoto wa wana wa Isrãîl kwamba «mnyonyeshe ukiwa mtulivu, na pindi uogopapo kujulikana mambo yake, muweke sandukuni na ulitupe kwenye mto wa Nail bila ya kuogopa kwamba firáwn na watu wake watamuua na bila ya kuwa na masikitiko ya kutengana naye, hakika sisi tutamrudisha kwako na tutamtumiliza kuwa Mtume».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net