Al-Qasas 28:6
القصصوَنُمَكِّنَ لَهُمْ فِى ٱلْأَرْضِ وَنُرِىَ فِرْعَوْنَ وَهَـٰمَـٰنَ وَجُنُودَهُمَا مِنْهُم مَّا كَانُوا۟ يَحْذَرُونَ
Na kuwaimarisha katika ardhi, na kutokana na wao kuwaonyesha kina Firauni na Hamana na majeshi yao mambo yale waliyokuwa wakiyaogopa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kuwapa nguvu katika nchi, na kutokana na wao kuwaonyesha kina Firauni na Hamana na majeshi yao mambo yale waliyo kuwa wakiyaogopa. [6]
[6] Na tuwathibitishe katika nchi, na wawe na pahali pao humo. Na tuwathibitishie Firauni na Hamana na majeshi yao yale waliyo kuwa wakiyakhofu, nayo ni kuondoka ufalme wake kwa mkono wa mwenye kuzaliwa katika Wana wa Israili.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tuwape uthabiti katika nchi na tumfanye Firáwn, Hāmān na askari wao waone, kutoka kundi hili linalonyongeshwa kile walichokuwa wakikiogopa cha kuangamia kwao, na kuondoka ufalme wao, na kuwatoa wao kwenye nyumba zao kwa mkono wa mzaliwa wa Wana wa Isrãîl.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net