Al-Qasas 28:67
القصصفَأَمَّا مَن تَابَ وَءَامَنَ وَعَمِلَ صَـٰلِحًا فَعَسَىٰٓ أَن يَكُونَ مِنَ ٱلْمُفْلِحِينَ
Ama mwenye kutubu na akaamini na akatenda mema, huyo atakuwa miongoni mwa wenye kufaulu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ama mwenye kutubu na akaamini na akatenda mema, huyo atakuwa miongoni mwa wenye kufanikiwa. [67]
[67] Hii ndiyo hali ya washirikina. Ama mwenye kutubu kutokana na shirki yake, na akaamini Imani ya kweli, na akatenda mema, basi huyo hutaraji kuwa kwa Mwenyezi Mungu miongoni mwa walio fuzu kuipata radhi ya Mwenyezi Mungu, na neema ya kudumu yenye kuendelea milele.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ama yule aliyetubia kati ya washirikina na akamtakasia Allah Mtukufu ibada na akafanya matendo yanayoambatana na amri Yake na Mtume Wake, yeye ni katika wale wanaofuzu katika Nyumba Mbili.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net