Al-Qasas 28:66
القصصفَعَمِيَتْ عَلَيْهِمُ ٱلْأَنۢبَآءُ يَوْمَئِذٍ فَهُمْ لَا يَتَسَآءَلُونَ
Basi zitawapotea habari siku hiyo, nao hawataulizana.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi zitawapotea khabari siku hiyo, nao hawataulizana. [66]
[66] Khabari hizo zikawapita hawazitambui kama kwamba ni vipofu. Ikawa hapana amuulizae mwenziwe, kwani wote walikuwa sawa sawa wameshindwa kujibu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hapo hoja zao zote zitafichika, wasijue ni hoja ipi waitumie. Wao hawatoulizana wao kwa wao kuhusu hoja za kuzitumia, maswali yenye nafuu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net