Al-Qasas 28:68
القصصوَرَبُّكَ يَخْلُقُ مَا يَشَآءُ وَيَخْتَارُ ۗ مَا كَانَ لَهُمُ ٱلْخِيَرَةُ ۚ سُبْحَـٰنَ ٱللَّهِ وَتَعَـٰلَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ
Na Mola wako Mlezi huumba na huteua atakavyo. Viumbe hawana hiari. Mwenyezi Mungu ametukuka na ametakasika na hao wanaowashirikisha naye.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Mola wako Mlezi huumba na huteuwa atakavyo. Viumbe hawana khiari. Mwenyezi Mungu ametukuka na ametakasika na hao wanao washirikisha naye. [68]
[68] Na Mola wako Mlezi anaumba atakalo kwa uwezo wake. Na anamkhitari amtakaye kwa hikima yake kumpa Ujumbe na ut'iifu kwa kujua kwake mwenyewe kufaa kwao. Wala hawawezi viumbe, na wala si haki, kumchagulia Mwenyezi Mungu walitakalo katika dini potovu, na miungu ya uwongo. Mtukufu ametakasika shani yake na washirika.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Mola wako anaumba anachokitaka kukiumba, na anamteua awe karibu na Yeye Anayemtaka katika viumbe wake. Na hakuna yoyote mwenye chochote cha amri na uteuzi. Kwa hakika, hilo ni la Allah Mtukufu Peke Yake, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Ametukuka na kutakasika na ushirikina wao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net