Al-Qasas 28:63
القصصقَالَ ٱلَّذِينَ حَقَّ عَلَيْهِمُ ٱلْقَوْلُ رَبَّنَا هَـٰٓؤُلَآءِ ٱلَّذِينَ أَغْوَيْنَآ أَغْوَيْنَـٰهُمْ كَمَا غَوَيْنَا ۖ تَبَرَّأْنَآ إِلَيْكَ ۖ مَا كَانُوٓا۟ إِيَّانَا يَعْبُدُونَ
Watasema wale iliyothibiti juu yao kauli, "Mola wetu Mlezi! Hawa ndio tuliowapoteza. Tuliwapoteza kama tulivyopotea sisi. Tunajitenga nao mbele yako. Hawakuwa wakituabudu sisi."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Watasema wale iliyo thibiti juu yao kauli: Mola wetu Mlezi! Hawa ndio tulio wapoteza. Tuliwapoteza kama tulivyo potea sisi. Tunajitenga nao mbele yako. Hawakuwa wakituabudu sisi. [63]
[63] Watasema waongozi wa makafiri katika walio stahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na vitisho vyake: Ewe Mola wetu Mlezi! Hawa tulio waita kwenye shirki na tukawapambia upotovu tuliwapoteza. Kwa sababu wao walikhiari ukafiri na wakaupokea, kama sisi tulivyo ukhiari na tukaupokea. Leo sisi tunajitenga nao kwako na ukafiri walio ukhiari duniani. Hawakuwa wao wakituabudu sisi; bali wakiabudu pumbao zao, na wakit'ii matamanio yao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Watasema wale ambao imethibiti kwao adhabu, nao ni walinganizi wa ukafiri, «Mola wetu! Hawa ndio tuliowapoteza. Tuliwapoteza kama tulivyopotea sisi. tumejitakasa kwako na urafiki wao na uokoaji wao. Hawakuwa ni sisi wanaotuabudu, Hakika ni kwamba wao walikuwa wakiwaabudu mashetani».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net