Al-Qasas 28:62
القصصوَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ أَيْنَ شُرَكَآءِىَ ٱلَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ
Na siku atakapowaita na akasema, "Wako wapi mliokuwa mkidai kuwa ni washirika wangu?"
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na siku atakapo waita na akasema: Wako wapi mlio kuwa mkidai kuwa ni washirika wangu? [62]
[62] Ewe Mtume! Kumbuka siku watapo simama hawa mbele ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuhisabiwa, naye Subhanahu akawaita kwa kuwatahayarisha: Wako wapi hao miungu mlio dai kuwa ni washirika wangu, wapate kukuteteeni na kukuombeeni?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na siku ambayo Allah Mtukufu, Aliyetukuka na kuwa juu, Atakapowaita wale waliomshirikisha Yeye wategemewa na masanamu ulimwenguni, awaambie, «Wako wapi washirika wangu ambao nyinyi mlikuwa mkidai kuwa wao ni washirika wangu?»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net