Al-Qasas 28:61
القصصأَفَمَن وَعَدْنَـٰهُ وَعْدًا حَسَنًا فَهُوَ لَـٰقِيهِ كَمَن مَّتَّعْنَـٰهُ مَتَـٰعَ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا ثُمَّ هُوَ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ مِنَ ٱلْمُحْضَرِينَ
Je, yule tuliyemuahidi ahadi nzuri, tena naye akayapata, ni kama tuliyemstarehesha kwa starehe za maisha ya duniani, na kisha Siku ya Kiyama akawa miongoni mwa wanaohudhurishwa?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je! Yule tuliye muahidi ahadi nzuri, tena naye akayapata, ni kama tuliye mstarehesha kwa starehe za maisha ya duniani, na kisha Siku ya Kiyama akawa miongoni mwa wanao hudhurishwa? [61]
[61] Hawi sawa mwenye kuamini na akatenda mema na akastahiki ahadi ya Mwenyezi Mungu na ahadi ya malipo mema na Pepo, na akayapata kama alivyo muahidi Mwenyezi Mungu; kulingana huyu na yule aliye kanusha na akatenda vitendo viovu, na yakamzuga maisha ya dunia na mapambo yake, na kisha Siku ya Kiyama akawa katika walio hudhurishwa kwa ajili ya hisabu, na akawa katika wenye kuhiliki kwa adhabu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Je, yule tuliyomuahidi Pepo, miongoni mwa viumbe wetu, kwa sababu ya kututii, akawa ni mwenye kupata alichoahidiwa na ni mwenye kukifikia, ni kama yule tuliyempa, katika uhai wa kilimwengu, starehe zake, naye akastarehe nazo na akaipa mbele ladha ya karibu kuliko ile ya baadaye, kisha yeye akawa ni mwenye kuhudhurishwa Siku ya Kiyama ili ahesabiwe na alipwe? Makundi mawili haya hayalingani. Basi mwenye akili ajichagulie nafsi yake kile kilicho bora kuchagua, nacho ni kule kumtii Allah Mtukufu na kutafuta radhi Zake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net