Al-Qasas 28:60
القصصوَمَآ أُوتِيتُم مِّن شَىْءٍ فَمَتَـٰعُ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا وَزِينَتُهَا ۚ وَمَا عِندَ ٱللَّهِ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰٓ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ
Na chochote mlichopewa, ni matumizi ya maisha ya dunia na pambo lake. Na yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ndiyo bora na yatakayobaki zaidi. Basi je, hamfahamu?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na chochote mlicho pewa ni matumizi ya maisha ya dunia na pambo lake. Na yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ndio bora na yatakayo baki zaidi. Basi je, hamfahamu? [60]
[60] Na kila kitu mlicho ruzukiwa katika starehe za dunia na mapambo yake kina ukomo wake kwa muda mfupi. Hayo yasikuzuieni kuamini na kutenda vitendo vyema. Kwani hakika yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu huko Akhera, nayo ni thawabu na neema za milele, yana nafuu zaidi, na yana dawamu kuliko hayo yote. Basi kwa nini hamtumii akili zenu badala ya pumbao zenu?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na chochote kile mlichopewa, enyi watu, cha mali na watoto, basi hayo ni starehe ya nyinyi kustarehe nayo katika maisha haya ya kilimwengu na ni pambo la kujipamba nalo. Na yaliyoko kwa Allah Mtukufu, yaliyowekewa watu walio watiifu Kwake na wenye kumtegemea, ni bora zaidi na ni yenye kusalia zaidi, kwani hayo ni ya daima yasiyomalizika. Basi nyinyi hamuwi na akili, enyi watu, ya kuzingatia kwayo, mkajua jema na ovu?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net