Al-Qasas 28:59
القصصوَمَا كَانَ رَبُّكَ مُهْلِكَ ٱلْقُرَىٰ حَتَّىٰ يَبْعَثَ فِىٓ أُمِّهَا رَسُولًا يَتْلُوا۟ عَلَيْهِمْ ءَايَـٰتِنَا ۚ وَمَا كُنَّا مُهْلِكِى ٱلْقُرَىٰٓ إِلَّا وَأَهْلُهَا ظَـٰلِمُونَ
Na Mola wako Mlezi haangamizi miji mpaka ampeleke Mtume katika miji yake mikuu awasomee Ishara zetu. Wala hatuiangamizi miji mpaka watu wake wawe madhalimu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Mola wako Mlezi haangamizi miji mpaka ampeleke Mtume katika miji yake mikuu awasomee Ishara zetu. Wala hatuiangamizi miji mpaka watu wake wawe madhaalimu. [59]
[59] Na haikuwa katika hikima ya Mwenyezi Mungu Mtukufu - naye ndiye Mola wako Mlezi aliye kuumba na kukuteuwa - kuiangamiza miji mikubwa ila baada ya kuwapelekea watu wake Mtume mwenye miujiza iliyo wazi awasomee Kitabu kilicho teremshwa, na awabainishie sharia, na kisha wawe hawaamini. Wala Sisi hatuangamizi miji mikubwa ila wakiwa watu wake wanaendelea na udhalimu na uadui.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hakuwa Mola wako, ewe Mtume, ni mwenye kuiangamiza miji iliyo pembezoni mwa Makkah katika zama zako mpaka atume kwenye kilele cha miji hiyo, nacho ni Makkah, Mtume atakayewasomea wao aya zetu. Na hatukuwa ni wenye kuiangamiza miji isipokuwa na watu wake wanajidhulumu wenyewe kwa kumkanusha Allah Mtukufu na kumuasi, basi wao kwa hivyo wanastahili mateso na adhabu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net