Al-Qasas 28:58
القصصوَكَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَرْيَةٍۭ بَطِرَتْ مَعِيشَتَهَا ۖ فَتِلْكَ مَسَـٰكِنُهُمْ لَمْ تُسْكَن مِّنۢ بَعْدِهِمْ إِلَّا قَلِيلًا ۖ وَكُنَّا نَحْنُ ٱلْوَٰرِثِينَ
Na miji mingapi iliyojifahirisha katika maisha yao tumeiangamiza! Na hayo maskani yao hayakukaliwa tena baada yao, isipokuwa kwa uchache tu. Na Sisi ndio tumekuwa warithi wao.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na miji mingapi iliyo jifakharisha tumeiangamiza! Na hayo maskani yao hayakukaliwa tena baada yao, ila kwa uchache tu. Na Sisi ndio tumekuwa warithi wao. [58]
[58] Watu hawa hawazingatii yaliyo wapata kaumu zilizo kwisha tangulia. Iliangamizwa miji ya walio ghurika na neema za Mwenyezi Mungu, na kisha wakazikanusha na wakamkanusha Mwenyezi Mungu. Na haya majumba yao yamekuwa matupu, magofu, hayafai kukaliwa ila nadra tu kwa wapita njia. Na yamebaki hayana mwenye kuyamiliki baada yao ila Mwenyezi Mungu Mwenye utukufu na ukarimu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wengi miongoni mwa watu wa miji tuliwaangamiza yalipowapumbaza wao maisha yao yakawashughulisha wasiwaamini Mitume, kwa hivyo wakakufuru na wakapita kiasi. Basi hayo ndio majumba yao, hayakukaliwa baada yao isipokuwa machache katika hayo. Na sisi daima ndio wenye kuwarithi waja: tunawafisha, kisha wanarejea kwetu tukawalipa kwa matendo yao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net