Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 57

Al-Qasas 28:57

القصص

وَقَالُوٓا۟ إِن نَّتَّبِعِ ٱلْهُدَىٰ مَعَكَ نُتَخَطَّفْ مِنْ أَرْضِنَآ ۚ أَوَلَمْ نُمَكِّن لَّهُمْ حَرَمًا ءَامِنًا يُجْبَىٰٓ إِلَيْهِ ثَمَرَٰتُ كُلِّ شَىْءٍ رِّزْقًا مِّن لَّدُنَّا وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ

Maana

Na wakasema, "Tukiufuata uwongofu huu pamoja nawe, tutanyakuliwa kutoka nchi yetu." Je, kwani Sisi hatukuwaweka imara katika pahala patakatifu, penye amani, ambapo huletewa matunda ya kila aina kuwa ni riziki itokayo kwetu? Lakini wengi wao hawajui.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wakasema: Tukiufuata uwongofu huu pamoja nawe tutanyakuliwa kutoka nchi yetu. Je! Kwani Sisi hatukuwaweka imara katika pahala patakatifu, penye amani, ambapo huletewa matunda ya kila aina kuwa ni riziki itokayo kwetu? Lakini wengi wao hawajui. [57]

[57] Na washirikina wa Makka walimwambia Mtume s.a.w. kwa kujitolea udhuru kwa kubakia kwao katika dini yao: Tukikufuata wewe katika dini yako Waarabu watatutoa katika nchi yetu, na watatushinda katika utawala wetu. Na hakika wao ni waongo katika kutoa udhuru wao huo. Kwani Mwenyezi Mungu alikuwa kawaweka imara na madhubuti katika nchi yao. Na akaifanya nchi takatifu yenye amani, hawashambuliwi wala hawauwawi, na hali wao ni makafiri. Na wanaletewa matunda na kheri nyengine za aina nyingi, ambazo Mwenyezi Mungu anawaletea kutoka kila upande. Basi huwaje awaondolee amani, na awaachilie wakinyakuliwa wakiongeza juu ya utakatifu wa Nyumba ya Alkaaba Imani kumuamini Muhammmad! Lakini wengi wao hawaijui Haki. Lau kuwa wanaijua wasinge khofu kunyakuliwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na makafiri wa Makkah wanasema, «Tukiifuata haki uliyotuletea na tukajiepusha na wategemewa na waungu, tutanyakuliwa kutoka kwenye ardhi yetu kwa kuuawa na kutekwa na kuporwa mali.» Kwani hatukuwafanya wao wamakinifu ndani ya mji wa amani, ambao ndani yake tumeharamisha umwagaji damu na ambao yanaletwa huko matunda ya kila aina yakiwa ni riziki kutoka kwetu? Lakini wengi wa hawa washirikina hawajui kadiri ya neema hizi kwao, wakapata kumshukuru Aliyewaneemesha wao kwazo na wakamtii.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net