Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 56

Al-Qasas 28:56

القصص

إِنَّكَ لَا تَهْدِى مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَـٰكِنَّ ٱللَّهَ يَهْدِى مَن يَشَآءُ ۚ وَهُوَ أَعْلَمُ بِٱلْمُهْتَدِينَ

Maana

Kwa hakika, wewe humwongoi umpendaye. Lakini Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye. Na Yeye ndiye anawajua zaidi waongokao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kwa hakika wewe humwongoi umpendaye, lakini Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye. Na Yeye ndiye anawajua zaidi waongokao. [56]

[56] Ewe Mtume! Hakika wewe una pupa sana kutaka hawa watu wako waongoke. Lakini wewe huwezi kumuingiza katika Uislamu kila umpendaye. Lakini Mwenyezi Mungu humwongoa kuendea Imani yule anaye mjua kuwa ameelekea uwongofu na ameukhiari. Na Yeye ndiye Mwenye kujua, wala hapana ajuaye zaidi kuliko Yeye, nani atakaye ingia katika safu za wenye kuongoka.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wewe, ewe Mtume, humuongoi, uongofu wa kumuafikia, unayependa aongoke. Lakini hilo liko kwenye mkono wa Allah Mtukufu, Anamuongoa Anayemtaka kumuongoa kwenye Imani na kumuafikia aifuate. Na Yeye Ndiye Anayemjua zaidi anayefaa kuongoka, hivyo basi Anamuongoa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net