Al-Qasas 28:55
القصصوَإِذَا سَمِعُوا۟ ٱللَّغْوَ أَعْرَضُوا۟ عَنْهُ وَقَالُوا۟ لَنَآ أَعْمَـٰلُنَا وَلَكُمْ أَعْمَـٰلُكُمْ سَلَـٰمٌ عَلَيْكُمْ لَا نَبْتَغِى ٱلْجَـٰهِلِينَ
Na wanaposikia upuuzi, hujitenga nao na husema, "Sisi tuna vitendo vyetu, na nyinyi mna vitendo vyenu. Salamun Alaikum (Amani iwe juu yenu)! Sisi hatutaki kujibizana na wajinga."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wanapo sikia upuuzi hujitenga nao na husema: Sisi tuna vitendo vyetu, na nyinyi mna vitendo vyenu. Salamun Alaikum, Amani juu yenu! Sisi hatutaki kujibizana na wajinga. [55]
[55] Na wanapo sikia upotovu wa wajinga hujitenga mbali nao, kwa kujiepusha na kuondoka, na husema: Sisi tuna a'mali yetu na hatuiachi, na nyinyi mna a'mali yenu ya upotovu na madhambi yake yapo juu yenu. Na sisi tunakuacheni na mambo yenu, kwani sisi hatupendi kusuhubiana na majaahili.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wanaposikia, watu hawa, maneno ya ubatilifu, hawayasikilizi, na wanasema, «Sisi tuna matendo yetu tusiyoyaacha, na nyinyi mna matendo yenu msiyoyaacha. Sisi hatujishughulishi kuwajibu nyinyi, na hamtasikia kutoka kwetu isipokuwa mema, na hatutasema na nyinyi kulingana na ujinga wenu, kwa kuwa sisi hatutaki njia ya wajinga na hatuipendi.» Na haya ni miongoni mwa maneno mazuri zaidi ambayo wanao lingania kwa Allah Mtukufu wanayasema.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net