Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 64

Al-Qasas 28:64

القصص

وَقِيلَ ٱدْعُوا۟ شُرَكَآءَكُمْ فَدَعَوْهُمْ فَلَمْ يَسْتَجِيبُوا۟ لَهُمْ وَرَأَوُا۟ ٱلْعَذَابَ ۚ لَوْ أَنَّهُمْ كَانُوا۟ يَهْتَدُونَ

Maana

Na itasemwa, "Waiteni hao miungu wa kishirikina wenu!" Basi watawaita, lakini hawatawaitikia, na wataiona adhabu; laiti wangelikuwa wameongoka!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na itasemwa: Waiteni hao miungu wa kishirikina wenu! Basi watawaita, lakini hawatawaitikia, na wataiona adhabu; laiti wangeli kuwa wameongoka! [64]

[64] Na Mwenyezi Mungu kuwaamrisha makafiri ni kwa kuwatahayarisha tu, kwa vile kuwataka wawaite wale miungu ya ushirikina wawaokoe na adhabu yake, kama walivyo dai. Wakaitikia kwa unyonge, na wakawaita kwa kuwa hawana hila. Wasipate jawabu yoyote. Wakaiona adhabu walio ahidiwa iko mbele yao, na wakatamani lau kuwa katika dunia yao wangeli kuwa Waumini walio ongoka, jinsi ya adhabu iliyo wafikia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wataambiwa, Siku ya Kiyama, wale wenye kumshirikisha Allah Mtukufu, «Waiteni washirika wenu ambao mlikuwa mkiwaabudu badala ya Allah Mtukufu.» Na wao wakawaita na wasiwajibu. Na wakaiona wazi adhabu, na lau wao wangekua waongofu ulimwenguni, wasingeadhibiwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net