Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 50

Al-Qasas 28:50

القصص

فَإِن لَّمْ يَسْتَجِيبُوا۟ لَكَ فَٱعْلَمْ أَنَّمَا يَتَّبِعُونَ أَهْوَآءَهُمْ ۚ وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّنِ ٱتَّبَعَ هَوَىٰهُ بِغَيْرِ هُدًى مِّنَ ٱللَّهِ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Maana

Na ikiwa hawakuitikii, basi jua kuwa wanafuata matamanio yao tu. Na ni nani aliyepotea zaidi kumshinda anayefuata matamanio yake bila ya uongofu utokao kwa Mwenyezi Mungu? Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ikiwa hawakuitikii, basi jua kuwa wanafuata pumbao lao tu. Na nani aliye potea zaidi kumshinda anaye fuata pumbao lake bila ya uwongofu utokao kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu. [50]

[50] Na ikiwa hawaitikii wito wako kwa kuleta kitabu kiongofu zaidi, basi jua kuwa wamebanwa na hawakubakiliwa na hoja yoyote, na kwamba kwa hayo wanafuata pumbao zao tu. Na hapana aliye zidi kwa upotovu kuliko yule anaye fuata pumbao lake katika dini, bila ya uwongofu kutokana na Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu hamwafiki mwenye kuidhulumu nafsi yake kwa kufuata upotovu bila ya kuitafuta Haki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wasipokuitikia kwa kuleta Kitabu, na hawakusaliwa na hoja yoyote, basi ujue kwamba wao wanafuata matamanio yao. Na hakuna yoyote aliye mpotevu zaidi kuliko yule aliyefuata matamanio yake bila ya kuwa na uongofu kutoka kwa Allah Mtukufu. Hakika Allah Mtukufu hawapi taufiq kuifikia haki watu madhalimu walioenda kinyume na amri ya Allah Mtukufu na wakakiuka mipaka Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net