Al-Qasas 28:51
القصصوَلَقَدْ وَصَّلْنَا لَهُمُ ٱلْقَوْلَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ
Na sasa kwa yakini tumewafikishia Neno moja baada ya lingine ili wapate kukumbuka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na sasa kwa yakini tumewafikishia Neno ili wapate kukumbuka. [51]
[51] Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu amewateremshia Qur'ani kwa utungo, baadhi yake ikifuatia baadhi kwa mujibu wa inavyo takikana na hikima, na kulingana na ahadi, na maonyo, na hadithi, na mazingatio, ili wapate kupima na kuyaamini yaliomo ndani yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kwa hakika, tuliifafanua na kuieleza Qur’ani kwa kuwaonea huruma watu wako, ewe Mtume, huenda wao wakakumbuka na wakawaidhika nayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net