Al-Qasas 28:49
القصصقُلْ فَأْتُوا۟ بِكِتَـٰبٍ مِّنْ عِندِ ٱللَّهِ هُوَ أَهْدَىٰ مِنْهُمَآ أَتَّبِعْهُ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ
Sema, "Basi leteni Kitabu kinachotoka kwa Mwenyezi Mungu kilicho kiongofu zaidi kuliko hivi viwili nikifuate, kama nyinyi ni wakweli."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Basi leteni Kitabu kinacho toka kwa Mwenyezi Mungu chenye kuongoka zaidi kuliko hivi viwili tukifuate, kama nyinyi mnasema kweli. [49]
[49] Ewe Mtume! Waambie: Ikiwa hamuiamini Taurati na Qur'ani basi leteni kitabu kingine kinacho toka kwa Mwenyezi Mungu kilicho na uwongofu bora kuliko hivyo, au kama hivyo, nami nikifuate pamoja nanyi, ikiwa nyinyi mnasema kweli katika hayo madai yenu kwamba tuliyo kuja nayo ni uchawi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Waambie hawa, ewe Mtume, «Basi Leteni kitabu kinachotoka kwa Allah Mtukufu ambacho ni cha sawa zaidi kuliko Taurati na Qur’ani, nipate kukifuata mkiwa nyinyi ni wakweli katika madai yenu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net