Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 48

Al-Qasas 28:48

القصص

فَلَمَّا جَآءَهُمُ ٱلْحَقُّ مِنْ عِندِنَا قَالُوا۟ لَوْلَآ أُوتِىَ مِثْلَ مَآ أُوتِىَ مُوسَىٰٓ ۚ أَوَلَمْ يَكْفُرُوا۟ بِمَآ أُوتِىَ مُوسَىٰ مِن قَبْلُ ۖ قَالُوا۟ سِحْرَانِ تَظَـٰهَرَا وَقَالُوٓا۟ إِنَّا بِكُلٍّ كَـٰفِرُونَ

Maana

Ilipowajia Haki kutoka kwetu, walisema, "Mbona hakupewa kama aliyopewa Musa?" Je, kwani wao hawakuyakataa aliyopewa Musa zamani? Walisema, "Ni wachawi wawili wanasaidiana." Na wakasema, "Hakika sisi tunawakataa wote."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ilipo wajia Haki kutoka kwetu walisema: Mbona hakupewa kama aliyo pewa Musa? Je! Kwani wao hawakuyakataa aliyo pewa Musa zamani? Walisema: Ni wachawi wawili wanasaidiana. Na wakasema: Hakika sisi tunawakataa wote. [48]

[48] Na alipo ileta Mtume wa Mwenyezi Mungu Qur'ani kutokana na Mwenyezi Mungu, makafiri walisema: Laiti yeye angeli pewa miujiza ya kuonekana na kama aliyo pewa Musa, na Kitabu cha kuteremka mara moja kama Taurati! Na hali hao walimkataa Musa na Ishara zake, kama hivi leo wanavyo mkataa Muhammad na Kitabu chake, na wakasema: Sisi tunawakataa wote wawili. Basi kukataa ndiko kuliko pelekea kuikanya miujiza.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na alipowajia Muhammad watu hawa akiwa ni muonyaji kwao walisema, «Si apewe, huyu aliyetumwa kwetu, mfano wa kile alichopewa Mûsã, cha miujiza inayoonekana na Kitabu kilichoteremshwa mara moja.» Waambie, ewe Mtume, Je, si Mayahudi walikikanusha kile alicholetewa Mûsã hapo kabla? Walisema kwamba ndani ya Taurati na Qur’ani kuna aina mbili za uchawi zilizosaidiana katika uchawi utokanao na hivyo viwili, na wakasema, «Sisi ni wenye kuvikanusha vyote viwili».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net