Al-Qasas 28:47
القصصوَلَوْلَآ أَن تُصِيبَهُم مُّصِيبَةٌۢ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ فَيَقُولُوا۟ رَبَّنَا لَوْلَآ أَرْسَلْتَ إِلَيْنَا رَسُولًا فَنَتَّبِعَ ءَايَـٰتِكَ وَنَكُونَ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ
Na usije kuwasibu msiba kwa iliyoyatanguliza mikono yao, wakasema, "Ewe Mola wetu Mlezi, mbona hukututumia Mtume nasi, tukafuata Ishara zako, na tukawa miongoni mwa Waumini?"
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na usije kuwasibu msiba kwa iliyo yatanguliza mikono yao, wakasema: Ewe Mola wetu Mlezi! Mbona hukututumia Mtume nasi, tukafuata Ishara zako, na tukawa miongoni mwa Waumini? [47]
[47] Ingeli kuwa makafiri wanapo patwa na mateso kwa sababu ya ukafiri wao wakataka udhuru na wakadai wakisema: Ewe Mola wetu Mlezi! Mbona hukutuletea Mtume tukamuamini na tukaikubali miujiza yake nasi tukawa miongoni mwa Waumini, basi usinge kuwepo Ujumbe wa Mitume.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na lau ingewateremkia adhabu hawa makafiri kwa sababu ya ukafiri wao, wangesema, «Si ilikua utuletee kwaza Mtume kwetu, tupate kuzifuata aya zako zilizoteremshwa kwenye Kitabu chako na tuwe ni miongoni mwa wenye kukuamini?»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net