Al-Qasas 28:46
القصصوَمَا كُنتَ بِجَانِبِ ٱلطُّورِ إِذْ نَادَيْنَا وَلَـٰكِن رَّحْمَةً مِّن رَّبِّكَ لِتُنذِرَ قَوْمًا مَّآ أَتَىٰهُم مِّن نَّذِيرٍ مِّن قَبْلِكَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ
Wala hukuwa kando ya mlima ule tuliponadi. Lakini ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi ili uwaonye watu wasiopata kufikiwa na mwonyaji kabla yako, huenda wakakumbuka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala hukuwa kando ya mlima tulipo nadi. Lakini ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi ili uwaonye watu wasio pata kufikiwa na mwonyaji kabla yako, huenda wakakumbuka. [46]
[46] Wala wewe, ewe Mtume, hukuwepo hapo kando ya mlima pale Mwenyezi Mungu alipo mwita Musa na akamteuwa kumpa Utume wake. Lakini Mwenyezi Mungu amekujuvya haya kwa njia ya wahyi (ufunuo), kutokana na rehema yake kwako na kwa umma wako, wapate kufikisha hayo kwa kaumu ambayo haikupata kufikiwa na Mtume kabla yako wewe, ili wakumbuke.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hukuwako, ewe Mtume, upande wa jabali la Ṭūr tulipomuita Mûsã, na hukushuhudia lolote katika hayo. Lakini sisi tulikupa utume ukiwa ni rehema kutoka kwa Mola wako, ili uwaonye watu ambao hawakujiwa na muonyaji kabla yako, huenda wao wakakumbuka wema uliokuja nao wakaufuata na uovu ulioukataza wakajiepusha nao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net