Al-Qasas 28:45
القصصوَلَـٰكِنَّآ أَنشَأْنَا قُرُونًا فَتَطَاوَلَ عَلَيْهِمُ ٱلْعُمُرُ ۚ وَمَا كُنتَ ثَاوِيًا فِىٓ أَهْلِ مَدْيَنَ تَتْلُوا۟ عَلَيْهِمْ ءَايَـٰتِنَا وَلَـٰكِنَّا كُنَّا مُرْسِلِينَ
Lakini Sisi tuliziumba kaumu, na ukawa mrefu umri juu yao. Wala hukuwa mkazi na watu wa Madyana ukiwasomea Aya zetu. Lakini ni Sisi tuliokuwa tukiwatuma Mitume.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Lakini Sisi tuliziumba kaumu, na ukawa mrefu umri juu yao. Wala hukuwa mkaazi na watu wa Madyana ukiwasomea Aya zetu. Lakini ni Sisi tulio kuwa tukiwatuma Mitume. [45]
[45] Na lakini Sisi tumeziumba kaumu nyingi katika vizazi vilivyo pitiwa na zama ndefu, hata wakasahau maagano yaliyo chukuliwa kwao. Na wewe, ewe Mtume, hukuwa mkaazi wa Madyana hata ndio uwasimulie watu wa Makka khabari zao. Lakini Sisi tumekutuma wewe, na tumekupa khabari zao kwa njia ya wahyi (Ufunuo).
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Lakini sisi tuliwaumba watu baada ya Mûsã, wakakaa kwa muda mrefu, wakasahau ahadi ya Allah Mtukufu, wakaacha amri yake. Wala hukuwa ni miongoni mwa wakazi wa mji wa Madyan ukiwasomea kwao Kitabu chetu, na kwa hivyo ikakujia habari yao na ukaisimulia. Lakini habari uliokuja nayo kuhusu Mûsã ni wahyi na ni ushahidi wa utume wako.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net