Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 44

Al-Qasas 28:44

القصص

وَمَا كُنتَ بِجَانِبِ ٱلْغَرْبِىِّ إِذْ قَضَيْنَآ إِلَىٰ مُوسَى ٱلْأَمْرَ وَمَا كُنتَ مِنَ ٱلشَّـٰهِدِينَ

Maana

Wala wewe hukuwa upande wa magharibi tulipompa Musa amri, wala hukuwa katika waliohudhuria.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala wewe hukuwa upande wa magharibi tulipo mpa Musa amri, wala hukuwa katika walio hudhuria. [44]

[44] Wala wewe Muhammad, hukuwa na Musa upande wa magharibi wa huo mlima, pale Mwenyezi Mungu alipo agana naye kumuamrisha Ujumbe. Wala hukuishi zama za Musa, wala hukushuhudia alipo fikisha Utume. Basi vipi hawa watu wako wanakanusha Utume wako na wewe unawasomea khabari za walio tangulia?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hukuwako, ewe Mtume, upande wa jabali la jua la kuchwa wa Mûsã, tulipombebesha maamrisho yetu na makatazo yetu, na hukuwa ni kati ya wale waliolishuhudia hilo mpaka kusemwe kwamba habari hii imekufikia kwa njia hii.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net