Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 43

Al-Qasas 28:43

القصص

وَلَقَدْ ءَاتَيْنَا مُوسَى ٱلْكِتَـٰبَ مِنۢ بَعْدِ مَآ أَهْلَكْنَا ٱلْقُرُونَ ٱلْأُولَىٰ بَصَآئِرَ لِلنَّاسِ وَهُدًى وَرَحْمَةً لَّعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ

Maana

Na hakika bila ya shaka tulimpa Musa Kitabu baada ya kwisha kuziangamiza kaumu za mwanzo, ili kiwafumbue macho watu, na kiwe uongofu, na rehema, ili wapate kukumbuka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hakika bila ya shaka tulimpa Musa Kitabu baada ya kwisha ziangamiza kaumu za mwanzo, ili kiwafumbue macho watu, na kiwe uwongofu, na rehema, ili wapate kukumbuka. [43]

[43] Na kwa yakini Mwenyezi Mungu alimteremshia Musa Taurati, baada ya kuwahiliki wakanushao katika kaumu zilizo tangulia, ili iwe nuru ya nyoyo. Kwani nyoyo hizo zilikuwa gizani, haziijui Haki wala uwongozi mwema. Kwani hao walikuwa wakitangatanga tu katika upotovu, na hawaijui njia ya kupatia rehema kwa mwenye kutenda kwa ajili yake, na wakawaidhika kwa yaliyomo katika hiyo Taurati, na wakakimbilia kuzifuata amri, na kuyaacha yaliyo katazwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hakika tulimpa Mûsã Taurati baada ya kuwaangamiza ummah waliokuwa kabla yake, kama vile watu wa Nūḥ, ‘Ᾱd, Thamūd, na watu wa Lūṭ na watu wa Madyan, hali ya kuwa Taurati ina hoja kwa Wana wa Isrāil ambazo kwa hizo wanayaona yale yanayowafaa na yanayowadhuru, na ndani yake kuna rehema kwa wanaoifuata Taurati kivitendo. Huenda wao wakazikumbuka neema za Mweyezi Mungu juu yao, wakamshukuru kwa hizo na wasimkanushe.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net