Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 42

Al-Qasas 28:42

القصص

وَأَتْبَعْنَـٰهُمْ فِى هَـٰذِهِ ٱلدُّنْيَا لَعْنَةً ۖ وَيَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ هُم مِّنَ ٱلْمَقْبُوحِينَ

Maana

Na tukawafuatishia laana katika dunia hii, na Siku ya Kiyama watakuwa miongoni mwa wanaochusha.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tukawafuatishia laana katika dunia hii, na Siku ya Kiyama watakuwa miongoni mwa wanao chusha. [42]

[42] Na tukawafanya katika dunia hii wenye kupata laana, yaani wenye kutolewa wasiipate rehema yetu; na Siku ya Kiyama watakuwa miongoni mwa walio angamizwa. Na yaliyo simuliwa katika Aya mbili hizi juu yao ni dalili ya ghadhabu ya Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na tukamfuatilizia Firáwn na watu wake laana na hasira kutoka kwetu juu yao. Na Siku ya Kiyama, wao watakuwa ni miongoni mwa wale ambao matendo yao yalikuwa yamechafuka, wale watakaowekwa mbali na rehema za Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net