Al-Qasas 28:41
القصصوَجَعَلْنَـٰهُمْ أَئِمَّةً يَدْعُونَ إِلَى ٱلنَّارِ ۖ وَيَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ لَا يُنصَرُونَ
Na tuliwafanya ni waongozi waitao kwenye Moto. Na Siku ya Kiyama hawatanusuriwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tuliwafanya ni waongozi waitao kwenye Moto. Na Siku ya Kiyama hawatanusuriwa. [41]
[41] Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: Na tukawafanya hao ni wenye kuitia watu kwenye ukafiri, ambao khatima yake ni Moto. Na Siku ya Kiyama hawampati wa kuwanusuru na kuwatoa kwenye adhabu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tumemfanya Firáwn na watu wake ni wenye kuongoza kwenye njia ya motoni, wakifuatwa na watu wa ukafiri na uasi. Na Siku ya Kiyama hawataokolewa. Hiyo ni kwa sababu ya ukafiri wao na kuwakanusha kwao Mitume wa Mola wao na kuendelea kwao kufanya hivyo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net