Al-Qasas 28:40
القصصفَأَخَذْنَـٰهُ وَجُنُودَهُۥ فَنَبَذْنَـٰهُمْ فِى ٱلْيَمِّ ۖ فَٱنظُرْ كَيْفَ كَانَ عَـٰقِبَةُ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Basi tukamshika yeye na majeshi yake, na tukawatupa baharini. Basi hebu angalia ulikuwaje mwisho wa wenye kudhulumu?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi tukamshika yeye na majeshi yake, na tukawatupa baharini. Basi hebu angalia ulikuwaje mwisho wa wenye kudhulumu? [40]
[40] Tukamng'oa Firauni kwenye utawala wake, na tukawavutia taratibu yeye na majeshi yake mpaka baharini, na tukawazamisha na huku tunawatupia sababu ya dhulma yao. Basi zingatia, ewe Muhammad, na uwahadharishe watu wako watazame vipi unakuwa mwisho wa wenye kudhulumu katika dunia yao. Na hakika wewe ni mwenye kusaidiwa kupata ushindi juu yao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Tukamchukua Firáwn na askari wake tukawatupa wote baharini na tukawazamisha. Basi angalia, ewe Mtume, ulikuwa vipi mwisho wa hawa waliojidhulumu wenyewe wakamkanusha Mola wao?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net