Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 39

Al-Qasas 28:39

القصص

وَٱسْتَكْبَرَ هُوَ وَجُنُودُهُۥ فِى ٱلْأَرْضِ بِغَيْرِ ٱلْحَقِّ وَظَنُّوٓا۟ أَنَّهُمْ إِلَيْنَا لَا يُرْجَعُونَ

Maana

Na alipanda kiburi yeye na majeshi yake katika ardhi bila ya haki, na wakadhania kuwa hawatarudishwa kwetu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na alipanda kiburi yeye na majeshi yake katika nchi bila ya haki, na wakadhania kuwa hawatarudishwa kwetu. [39]

[39] Firauni na majeshi yake wakaendelea wakifanya kiburi katika nchi ya Misri kwa upotovu. Na wakadhani kuwa kabisa hawato fufuliwa Akhera kwa ajili ya hisabu na malipo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Firáwn na askari wake walifanya kiburi katika nchi ya Misri bila ya haki kwa kukataa kumuamini Mûsã na kumfuata katika lile alilowaitia na wakadhani kwamba baada ya kufa kwao hawatafufuliwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net