Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 38

Al-Qasas 28:38

القصص

وَقَالَ فِرْعَوْنُ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلْمَلَأُ مَا عَلِمْتُ لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرِى فَأَوْقِدْ لِى يَـٰهَـٰمَـٰنُ عَلَى ٱلطِّينِ فَٱجْعَل لِّى صَرْحًا لَّعَلِّىٓ أَطَّلِعُ إِلَىٰٓ إِلَـٰهِ مُوسَىٰ وَإِنِّى لَأَظُنُّهُۥ مِنَ ٱلْكَـٰذِبِينَ

Maana

Na Firauni akasema, "Enyi waheshimiwa, sijawahi kujua kama mnaye mungu asiyekuwa mimi. Ewe Haman, niwashie moto unichomee udongo, unijengee mnara nipate kumchungulia mungu wa Musa. Na hakika mimi ninamwona yeye ni katika waongo."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Firauni akasema: Enyi waheshimiwa! Sijui kama mnaye mungu asiye kuwa mimi. Ewe Haman! Niwashie moto unichomee udongo, unijengee mnara nipate kumchungulia mungu wa Musa. Na hakika mimi namwona yeye ni katika waongo. [38]

[38] Na Firauni alipo shindwa kuhojiana na Musa, na akaendelea na jeuri zake, alisema: Enyi wahishimiwa! Mimi sijui kama yupo mungu wenu mwenginewe isipo kuwa mimi. Na akamuamrisha waziri wake Haman amchomee matufali, na amjengee mnara mrefu apande, ende kumtazama huyo mungu anaye mlingania Musa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Firáwn akasema kuwaambia viongozi wa watu wake, «Enyi viongozi! Mimi sijui kwamba nyinyi mna mola isipokuwa mimi anayestahiki kuabudiwa. Basi, ewe Hāmān! Niwashie moto juu ya udongo mpaka ushikane, na unijengee jengo lenye urefu wa kuelekea juu, kwani huenda nikamchungulia muabudiwa wa Mûsã ambaye yeye anamuabudu na anawaita watu wamuabudu. Na mimi ninadhani kuwa yeye ni miongoni mwa warongo katika hayo anayoyasema».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net